Edward's blog

Narcotics Anonymous Tanzania (NATZ)

|

     Salamu na heri za sikukuu kutoka kwet hapa NATZ! Tunatumai tutaendelea kuwa pamoja katika mwaka mpya wa 2007, unaoanza rasmi baada ya masaa machache kutoka sasa hivi. Kwa upande wetu sisi hapa NATZ, tutaendelea kuhakikisha kuwa tunatimiza lengo kuu la NATZ - kumfikishia ujumbe wa tiba ya NATZ kila mlevi ambaye bado anateseka na kuteswa na ulevi.



Narcotics Anonymous (NA) Tanzania

|

   NA  Tanzania inatimiza mwezi mmoja tangu kuanzishwa. Ilikuwa mnamo tarehe 14 Novemba, 2006, siku ambayo Edward, Khadija na Stephane walianzisha NA Tanzania kwenye bwawa la Maweni, juu ya milima ya Usambara, kaskazini mashariki mwa Tanzania. Shukrani za dhati tunazielekeza kwa utawala na watumishi wa Maweni Farm Ltd, kwa kutengeneza mazingira yaliyowezesha tukio hilo.



Narcotics Anonymous (Tanzania)

|
Mila kumi na mbili za Narcotics Anonymous (NA)
Tunabaki na tulichonacho kwa kuwa macho na makini muda wote, na kama vile uhuru wa mtu unavyotokana na misingi au hatua kumi na mbili, basi uhuru wa kikundi unatokana na mila kumi na mbili.
Ili mradi vinavyotuunganisha ni imara kuliko vinvyotugawanyisha, yote ni njema.
1.



Narcotics Anonymous (NA) Tanzania

|

Misingi ya Narcotics Anonymous

Kama unataka tunachokigawa, na uko tayari kufanya jitihada kuipata, basi uko tayari kuchukua hatua fulani. Hii ni misingi iliyotuwezesha sisi kuushinda ulevi wetu.



Narcotics Anonymous, Tanzania

Leo asubuhi, pamoja na Stefan na Hadija, tumeanzisha Narcotics Anonymous (NA) ya kwanza Tanzania hapa Maweni.

Mlevi ni mtu ambaye maisha yake yanatawaliwa na vilevi kama vile sigara, pombe na madawa ya kulevya. Ulevi ni ugonjwa ambao hatma yake ni jela, hospitali na kifo. NA ni kikundi cha watu waliotambua kuwa ulevi ni tatizo kubwa. Sisi ni walevi tunaotafuta ahueni kwa kukutana mara kwa mara. NA inadhamiria kumwezesha mtu kutokutumia tena kilevi au vilevi. Kuna sharti moja tu la uanachama - nia ya kuacha ulevi. Tunashauri uwe wazi kimawazo na ujipe fursa ya kupata ahueni.



Syndicate content