Narcotics Anonymous Tanzania (NATZ)
Salamu na heri za sikukuu kutoka kwet hapa NATZ! Tunatumai tutaendelea kuwa pamoja katika mwaka mpya wa 2007, unaoanza rasmi baada ya masaa machache kutoka sasa hivi. Kwa upande wetu sisi hapa NATZ, tutaendelea kuhakikisha kuwa tunatimiza lengo kuu la NATZ - kumfikishia ujumbe wa tiba ya NATZ kila mlevi ambaye bado anateseka na kuteswa na ulevi.
Tangu kuanzishwa kwa NATZ mwezi uliopita tumefanikiwa kuzindua vikundi viwili vya NATZ. Kikundi cha kwanza kuzinduliwa ni kikundi cha "Waasisi", kilichozinduliwa Maweni na kukutana mara moja Chalinze na kukutana mara nyingine tena Uwanja wa Fisi. Kwa bahati mbaya, heka heka za kufungwa kwa Uwanja wa Fisi kwa amri ya Serikali kumesababisha "Waasisi", waliokuwa wanakutana katika hoteli ya Itongo, kukosa mahali pa kukutana. Hii imesababisha "Waasisi" kusitisha mikutano yao hadi hapo itakapopatikana sehemu nyingine ya kukutana. Taarifa za "Waasisi" zitaendelea kupatikana kwenye blog hii hii hapa, kwa hiyo tafadhali usichoke kutufuatilia.
Kikundi cha pili cha NATZ kuzinduliwa, mwezi mmoja baada ya kuanzishwa kwa NATZ na kikundi cha NATZ cha "Waasisi", ni kikundi cha NATZ cha "Wanamapinduzi". "Wanamapinduzi" wanakutana kila siku kuanzia saa kumi jioni hadi saa kumi na moja jioni kwenye mgahawa wa Kawawa, mkabala na hosteli ya Kijitonyama ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mtaa wa Nzasa, Mwenge, Dar es Salaam.
Wanamapinduzi, tangu kuanzishwa siku 17 zilizopita, wamezindua mikakati mikuu miwili yenye lengo la kufanikisha malengo ya NATZ
Mkakati wa kwanza ni kuanzisha na kuendesha "Nyumba ya Haki na Amani", itakayowapatia malazi ya muda walevi waliodhamiria kuachana na ulevi. Mkakati wa pili ni kuanzisha na kuendesha maonyesho ya kiutamaduni, hususan muziki, dansi, ngoma na maigizo, kila Jumamosi itakayorushwa hewani kwenye magazeti, redio, televisheni na kwenye mtandao wa internet. Onyesho litaitwa "BongoSplash!"
Kwa leo naishia hapa. Lakini usichoke kutufuatilia. Tunawatakia heri ya mwaka mpya wa 2007. Tuendelee kuwasiliana kwa kupitia edward@maweni.com. Kwaheri na heri ya msimu wa sikukuu!
comment
Attractive blogs always provide us some thing unique and innovative because are composition of different person’s ideas, comments and very authentic information that can change our life. I am Chris from New York and I have acquired the degree of MBIT from Oxford University, now days I am working on a very unique project of mcse certificaiton,that can make you successful and also can give you an attractive personality. I have inspired from your blog’information.after this project I will join your company.
here is some more info to
here is some more info to book report on the concerned content