Pombe kupita kiasi ni mbaya. Hebu angalia huyu mtu amepoteza fahamu na amelala bila yeye kujitambua katika Uwanja wa Fisi. Sisi tulijua ameshakufa na tulishindwa kumsaidia au kumshika kwa sababu tuliogopa tutashtakiwa baadaye. Kumbe, kesho yake tulisikia kwamba baada ya masaa kadhaa aliamka na kuweza kuondoka mwenyewe. Yeye ni mwuza machungwa sokoni ya Tandale na akishauza anakuja kulewa moja kwa moja. Pombe zinazouzwa kule ni kabunguz, mwamba, chibuko, pingu, dakika tatu, wanzuki ikiwemo na gongo. Haya ni baadhi ya matukio ya Uwanja wa Fisi usiku. Balaa tupu. Naomba hizi pombe zipitiwe na TBS.
Pombe kupita kiasi. Too much beer
Submitted by Elisa on Fri, 2006-11-17 22:52.
Media